Home Habari za michezo ACHANA NA STORI ZA UZUSHI….HUU HAPA UKWELI KUHUSU MUGALU NA TIMU YAKE...

ACHANA NA STORI ZA UZUSHI….HUU HAPA UKWELI KUHUSU MUGALU NA TIMU YAKE MPYA…LWANGA BADO SANA…


Aliyekua mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC, Chriss Mugalu (31) amejiunga na timu ya jeshi la anga la Iraq, Al Quwa Al-Jawaiya ambayo inashiriki ligi kuu nchini humo.

Mugalu ambaye ni raia wa Congo DR ni moja ya wachezaji walioachwa na Simba hivi karibuni baada ya pande zote mbili kufikia makubaliani.

Mugalu amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuwatumia wajeda hao wenye maskani yao katika wilaya ya Rusafa, Baghdad.

Wengine waliotemwa pamoja na Mugalu ni Medie Kagere ambaye tayari amesajiliwa na Singida Big Stars na Thadeo Lwanga ambaye bado hajajulikana anakwenda wapi.

SOMA NA HII  KWA SASA NI ZAMU YA STARS, ACHA KAZI IENDELEE