Home news KWA SASA NI ZAMU YA STARS, ACHA KAZI IENDELEE

KWA SASA NI ZAMU YA STARS, ACHA KAZI IENDELEE


MATOKEO ambayo yanapatikana uwanjani ni jitihada ambazo zinafanywa na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na uongozi bika kusahau mashabiki nao wananafasi yao pia.

Ni kawaida pale baada ya mechi kuisha wachezaji kujutia nafasi ambazo walizikosa huku mashabiki wakiwa hawana furaha kwa kuwa wamekosa kile walichotarajia kingeweza kutokea.

Sio mbaya makosa huwezi yaepuka ila yasiwe ni ya kujirudia mara kwa mara kama hali itakuwa hivyo hapo pana tatizo na lazima lifanyiwe kazi haraka sasa.

Tumeona na tumeshuhudia kwamba wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars walianza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Vizuri kuanza mapema na kulingana na ratiba ni kwamba leo Alhamisi wana kazi ya kusaka ushindi hapo ndipo uzuri ulipo.

Muda uwe ulikuwa ni mdogo ama mkubwa hakuna chaguo suala ni moja muhimu kupata matokeo na inawezekana kwa kuwa benchi la ufundi linajua namna ya kuwatumia wachezaji na kila mchezaji anajua majukumu yake.

Weka kando suala la kuongoza kundi hapa wimbo ni mmoja tu ambao unapaswa kuimbwa ushindi ushindi ushindi hakuna namna nyingine. 

Jana ilikuwa ni siku ya mwisho ya maandalizi basi kila kitu ninaamini kwamba kipo katika mpangilio mzuri na yale majukumu ambayo wachezaji mtapewa basi yafanyieni kazi kwa umakini.

Mkikumbuka kwamba mchezo wenu uliopita mlishinda na sasa mnapaswa kuendelea palepale mlipoishia na inawezekana kuwa hivyo tunawaamini.

Fanyeni kweli kutafuta ushindi, chezeni kwa juhudi isiyo ya kawaida na matokeo yataonekana baada ya dakika 90 pale mtakapokuwa mashujaa na taifa litashangilia pia.

Makosa ambayo mlifanya katika mchezo uliopita yawekeni kando lakini msiyapuuzie kwa kuyarudia msirudie songeni mbele vijana huku mkishirikiana.

Ukweli ni kwamba uwezo wa kushinda upo kwenye miguu yenu ya dhahabu na akili zenu ambazo mmepewa ni wajibu wenu kutimiza majukumu kwa ajili ya taifa la Tanzania. 

Kazi ya kwanza ikikamilika hapa nyumbani kituo kinachofuata ni ugenini na huko mmekuwa na rekodi mbovu katika kupata ushindi ipo wazi hata kwa mechi za kirafiki bado rekodi zinatukataa.

SOMA NA HII  WAKATI FEI TOTO AKIZIDI KUDENGUA...MUDATHIRI AITEKA 'SHOW' YANGA...NABI KAPAGAWA MAZIMA...

Kwa kuwa hilo tunalitambua basi kwa mechi ya nyumbani tuanze kupambana na kushinda ili ile ya marudio iwe ni sehemu ya kumalizia ile kazi tuliyoanzisha pale Uwanja wa Mkapa.

Vijana msisahau kwamba Watanzania wanawaamini na wapo pamoja nanyi na imani ni kwamba dua na maombi yao ni juu yenu kufanya vizuri. 

Ikiwa ni hivyo sasa kipi kitakachowafanya msipambambane kwa hali na mali kusaka ushindi ndani ya dakika 90 mkiwa katika uwanja uliojengwa kwa kodi za Watanzania?

Basi sawa ikiwa mtapambana matokeo yataonekana kwa kuwa mpira ni mchezo wa wazi na hakuna ambaye halitambui hilo hata wachezaji wenyewe wanajua.

Jambo la msingi ambalo nawakumbusha ni ishu ya nidhamu nje na ndani ya uwanja ni lazima iwe hivyo na kila mmoja atimize majukumu yake. 

Msiwadharau wapinzani wenu eti kwa kuwa mpo nyumbani hapana mnaweza kuwa nyumbani na mkaboroga vilevile, muhimu nidhamu na kujituma bila kuogopa.

Ushindi wa mapema utawapa nguvu ya kujiamini na kusonga mbele zaidi kila la kheri Stars acha kazi iendelee.