Home Habari za michezo WAKATI FEI TOTO AKIZIDI KUDENGUA…MUDATHIRI AITEKA ‘SHOW’ YANGA…NABI KAPAGAWA MAZIMA…

WAKATI FEI TOTO AKIZIDI KUDENGUA…MUDATHIRI AITEKA ‘SHOW’ YANGA…NABI KAPAGAWA MAZIMA…

Habari za Yanga

Umemuona kiungo Mudathir Yahya katika dakika zake 90 za kwanza kwenye ligi akiwa na uzi wa Yanga? Kama umeshangaa kiwango chake bora basi humzidi kocha wake Nasreddine Nabi ambaye ametuma salama ka wapinzani wake.

Akizungumza Nabi alisema kiwango cha Mudathir kimemshtua na bado haamini kama alikuwa anamuangalia mchezaji aliyekaa nje kwa miezi mitano bila kucheza soka akicheza kwa kiwango hicho.

Nabi alisema Mudathir ni kiungo shoka anayekaba mpaka kivuli cha mchezaji wa timu pinzani ambaye ameongezeka katika timu yake inayoongoza ligi ikiwa na pointi 53.

“Huyu ndiye kiungo mkabaji mwingine bora aliyeongezeka kwenye timu yetu, hiki kiwango alichokionyesha kimenishangaza sikuwa naamini kama ni mchezaji niliyeambiwa amekaa nje bila kucheza soka kwa miezi mitano,”alisema Nabi ambaye wakati wote alikuwa na uso wa furaha kubwa.

“Angalia anavyokaba kwa nguvu, ni mchezaji ambaye wakati wote anatamani mpira uwe katika umiliki wetu lakini muangalie anavyobadilika haraka kupiga pasi ndefu na fupi zinazofika.

“Nadhani bado kama nilivyokwambia anaweza kuwa bora zaidi ya hapa (Mudathir), tunaweza kumuongezea ubora kwa asilimia hamsini zaidi kwa hiki alichofanya jana (juzi),” alisema kocha huyo mahiri.

Aidha Nabi alisema baada ya ujio wa Mudathir sasa amepata kiungo ambaye hata akikosekana Khalid Aucho kuna mtu wa kuziba nafasi yake.

“Tulikuwa tunapata shida sana alipokuwa anakosekana Aucho, tulikuwa tunamuangalia Zawadi Mauya pekee, angalia wakati huu tunampata Mudathir huku Aucho na Mauya wako katika maumivu, huu ni usajili bora ambao tumeufanya sisi makocha na viongozi wa hii klabu.”

Mudathir ambaye alisajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili alicheza dakika 90 zake za kwanza kwenye ligi dhidi ya Ihefu na Yanga ikashinda kwa bao 1-0 na kuendelea kutamba juu ya msimamo wa ligi huku kiungo huyo akiwa katika kiwango bora.

SOMA NA HII  RASMI, KOCHA YANGA KUIBUKA BONGO KESHO