Home Habari za michezo TABIA ZA ‘KIWAKI’ ZAMPONZA MORRISON YANGA…NABI AMUONJESHA’ JOTO YA JIWE’…

TABIA ZA ‘KIWAKI’ ZAMPONZA MORRISON YANGA…NABI AMUONJESHA’ JOTO YA JIWE’…

Habari za Yanga

Mastaa watatu wa Yanga, wameonja joto la jiwe baada ya kusimamishwa na kocha Nasreddine Nabi kutokana na utovu wa nidhamu.

Mastaa hao ni Djuma Shaban, Farid Mussa na Benard Morrison ambao wamekosekana kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara, kutokana na utovu wa nidhamu.

BM33, Shaban Djuma na Farid Mussa ndio wachezaji ambao waliondolewa kikosini kutokana na kuchelewa kuripoti kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili.

Mastaa wote wa Yanga, walipewa mapumziko hayo baada ya kumaliza mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kilithibitisha kuwa, wachezaji hao walishindwa kuripoti kambini siku iliyokuwa inatakiwa siku iliyofuata waliporudi kocha Nabi aliwatimua.

“Wachezaji hao walizingua na kocha Nabi akawapa adhabu ya kimya kimya, ila tayari wameshaomba radhi na kurejeshwa kikosi na wameingia kambini na wenzao tayari kwa mchezo ujao dhidi ya Prisonms,” kimesema chanzo hicho kutoka ndani ya Yanga.

Wachezaji hao walizikosa mechi tatu za ligi dhidi ya Dodoma Jiji, Ihefu FC na Mbeya City ambapo Yanga ikishinda mbili na kupoteza mbele ya Ihefu na kukwamisha rekodi yao ya unbeaten iliyodumu kwa michezo 49 na kesho itashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Tanzania Prisons.

SOMA NA HII  ROBERTINHO:- SIMBA INAJULIKANA MPAKA BRAZILI...WATU WAIZUNGUMZIA SANA KULE...