Home Habari za michezo ROBERTINHO:- SIMBA INAJULIKANA MPAKA BRAZILI…WATU WAIZUNGUMZIA SANA KULE…

ROBERTINHO:- SIMBA INAJULIKANA MPAKA BRAZILI…WATU WAIZUNGUMZIA SANA KULE…

Habari za Simba leo

Robert Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anahitaji maboresho zaidi kwenye kikosi hicho ili kuongeza ushindani ndani ya timu hiyo.

Raia huyo wa Brazil amesema kuwa Simba ni timu kubwa ambayo inajulikana kila kona ya dunia hivyo ni muhimu kuwa na wachezaji wenye morali kubwa na ari ya upambanaji mwanzo mwisho.

Kocha huyo kwenye ligi kaongoza katika mechi 9 huku akiambulia sare katika mechi mbili dhidi ya Namungo na Azam FC zote ilikuwa kwa kufungana bao 1-1 baada ya kuchukua mikoba ya Zoran Maki.

Oliveira amesema:”Kwenye eneo la wachezaji ni muhimu kufanya maboresho kwa kuwa na wachezaji wakubwa wenye uwezo hii itakuwa sawa ndani ya kikosi kutokana na ukubwa wa Simba.

“Unajua Simba ni timu kubwa inajulikana hata Brazil wanaizungumzia Simba, Mali kila kona sasa tukiwa na wachezaji wazuri na wenye uwezo itakuwa rahisi kutupa matokeo na kuleta ushindani.

“Tumekuwa na mwendo ambao umekuwa mzuri lakini sio kwa kiasi kikubwa hii ilitokana na kuwa na wachezaji ambao ni majeruhi na adhabu za kadi zimekuwa zikifanya tusiwatumie wachezaji wengine,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS WADHAMIRIA KUFANYA MAAJABU KLABU BINGWA AFRIKA