Home Uncategorized MGHANA ALIYEKUBALI KUTUA YANGA APANIA KUZIFUNGA ZOTE ATAKAZOKUTANA NAZO

MGHANA ALIYEKUBALI KUTUA YANGA APANIA KUZIFUNGA ZOTE ATAKAZOKUTANA NAZO


MSHAMBULIAJI wa Rayon Sport ya Rwanda, Mghana, Michael Sarpong amefichua kuwa amekuwa akiskia ugumu wa Ligi Kuu Bara lakini haiwezi kumpa hofu kwani amepanga akitua tu Yanga basi atazifunga timu zote atakazokutana nazo ikiwemo Simba.
Mshambuliaji huyo kwa sasa amekuwa ni mchezaji huru baada ya Rayon kuvunja mkataba wake kutokana na madai ya utovu wa nidhamu licha ya msimu uliopita kufanikiwa kufunga mabao 16 yaliyosaidia kuipa ubingwa wa Rwanda.
Inaelezwa kuwa tayari Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na mwenyekiti wa timu hiyo, Dk Mshindo Msolla wamezungumza na wakala wa mshambuliaji huyo kwa ajili ya kujiunga na Yanga kutokana na mapendekezo ya kocha wao Mbelgiji, Luc Eymael.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Sarpong alisema kuwa licha kuwa wana ofa nyingi lakini kama atafanikiwa kujiunga na Yanga basi amepanga kuona anafunga katika kila mchezo atakaocheza kwa lengo la kuisaidia timu yake.
“Unajua mimi ni mchezaji na lengo la timu kuhitaji huduma yangu ni kwa sababu wameona ubora ambao nipo nao kitu ambacho natakiwa niwathibitishie ndani ya uwanja, mazungumzo yetu yanakwenda vizuri,” alisema.
SOMA NA HII  MOURINHO ABEBA MATUMAINI LIGI YA MABINGWA LICHA YA KICHAPO