Home Uncategorized MOURINHO ABEBA MATUMAINI LIGI YA MABINGWA LICHA YA KICHAPO

MOURINHO ABEBA MATUMAINI LIGI YA MABINGWA LICHA YA KICHAPO


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Spurs amesema kuwa bado wana nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na RB Leipzing ikiwa nyumbani.

Mourinho amesema kuwa zipo timu ambazo zimewahi kufungwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na walisonga mbele.

“Kuna timu nyingi ambazo zimewahi kufungwa kwenye Ligi ya Mabingwa kwenye mechi za nyumbani, hakuna mashaka kwa mchezo wetu wa marudio tutapambana kufanya vizuri,” amesema.


SOMA NA HII  MKALI WA KUMWAGA MAJI NDANI YA AZAM FC KUIKOSA MBEYA CITY LEO