Home Uncategorized BEKI MKENYA AJIPELEKA MWENYEWE SIMBA ASAINI

BEKI MKENYA AJIPELEKA MWENYEWE SIMBA ASAINI


MIKE Kibwage anayekipiga ndani ya KCB, raia wa Kenya ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Simba kuwa atakuja kuichezea timu hiyo kama watampa ofa nzuri.

Simba iko kwenye kazi kubwa ya kuhakikisha inasuka safu yake ya ulinzi ambayo Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck anaonekana kutoridhishwa nayo kwa madai inaruhusu mabao.
Kibwage anayekipiga KCB inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, ameweka wazi kuwa licha ya kuwa hajafuatwa rasmi na Simba lakini yuko tayari kutua kikosini humo na kufanya makubwa.
Beki huyo mwenye urefu wa futi sita, aliongeza kuwa kwa sasa ana mkataba ambao unaisha Oktoba, mwaka huu na kama Simba wakipeleka ofa nzuri basi hawezi kukataa na atapiga kazi vizuri tu.
“Nimesikia kuwa Simba wananitaka lakini hawajanifuata rasmi, hata hivyo niko tayari kuja kuichezea timu hiyo kama watakuja na ofa nzuri siwezi kuikataa,” amesema Mike.
SOMA NA HII  BILO AFUNGUKA MADUDU YANAYOFANYWA NA BOSS ALIANCE, KUMBE SUB ILIMFUKUZISHA KAZI BHANA