Home Uncategorized ISHU YA KONDE BOY NA WAWA KUREJEA SIMBA IPO HIVI

ISHU YA KONDE BOY NA WAWA KUREJEA SIMBA IPO HIVI

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu amesema kuwa nyota wake wawili wa kikosi cha kwanza ambao ni Pascal Wawa raia wa Ivory Coast na Luis Miqussone maarufu kama Konde Boy watarejea ndani ya wiki hii ili kukamilisha kikosi cha kwanza kwa ajili ya kujiandaa kutetea taji la Ligi Kuu Bara.

Agosti 22, kwenye kilele cha Simba day wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya Vital’O ya Burundi, wawili hao hawakuwepo kwenye utambulisho wa wachezaji kutokana na kupewa ruhusa kukamilisha masuala yao ya kifamilia ambapo inaelezwa kuwa walikwenda kuoa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa nyota hao ambao wamehusika kwenye jumla ya mabao sita ndani ya ligi kati ya 78 yaliyofungwa na Simba watarejea mapema kuendelea kazi ndani ya kikosi chake.

“Luis atarejea Jumanne,(Kesho), Wawa atarejea tarehe 26, baada ya hapo nitakuwa nimekamilisha kikosi kamili kwa ajili ya kuanza kufanya maandalizi ya msimu ujao kwa kuwa malengo yetu ni kutetea taji la Ligi Kuu Bara pamoja na malengo ambayo tumejiwekea ndani ya timu,” alisema.

Luis raia wa Msumbiji, alifunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao huku Wawa beki mwili jumba, raia wa Ivory Coast alitoa pasi moja ya bao.

SOMA NA HII  VIDEO: MTIBWA SUGAR SIMBA NI TIMU KUBWA AFRIKA, YAYEYUSHA NDOTO ZA UBINGWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here