Home news JE, YANGA NA SIMBA KUTOSHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO ?

JE, YANGA NA SIMBA KUTOSHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO ?

 


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameweka mkazo suala la  leseni za klabu akisisitiza kuwa, msimu ujao klabu itakayokuwa ikidaiwa haitaruhusiwa kucheza Ligi.

Karia amebainisha hayo leo Jumanne wakati wa wa kusaini mkataba wa haki za matangazo ya televisheni na Azam Media, jijini Dar es Salaam.

Amesema hakuna klabu itakayoruhusiwa kushiriki Ligi msimu ujao kama itakuwa na madeni, akisisitiza kwamba utaratibu wa leseni za klabu utazingatiwa ipasavyo.

“Klabu yenye madeni, hata iwe na imechukua ubingwa, msimu ujao haitaruhusiwa kushiriki Ligi kama itakuwa ina daiwa,” alisema.

Endapo, sheria hii itatekelezwa pengine baadhi ya klabu za ligi kuu, ikiwemo Yanga na Simba zinaweza kujikuta zikibanwa na kanuni hii kutokana na kuwa na madeni mengi kutoka kwa wachezaji wao.

Klabu ya Yanga na baadhi ya timu za ligi kuu zimekuwa zikilalamikiwa na wachezaji pamoja makocha kwa kushindwa kulipwa malipo yao kwa wakati .

Hivi Karibuni, klabu ya Biashara United ya Mara ililalamikiwa na baadhi ya wachezaji wake kwa kushindwa kuwalipa kwa wakati, aidha Aliekuwa kocha wa Gwambina FC, kabla ya kujiunga na Mtibwa Sugara, Ali Badru alinukuliwa na vyombo vya habari akilalamika kutokulipwa stahiki zake akiwa Gwambina.

Kwa Upande wa Yanga, kumekuwa na tetesi kuwa baadhi ya wachezaji wa sasa hawajilpwa stahiki zao za usajili wala mishahara hali inayopelkea kuwepo kwa matabaka kwa baadhi ya wachezaji.

Aidha Simba SC nao, wameingia kwenye doa hili,mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu, Sven Vandebroken kusemekaan akuwa amefungua shauri la mashtaka FIFA akitaka alipwe marupurupu na bonasi za msimu uliopita.

SOMA NA HII  KUWANIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE...SIMBA QUEENS WAIZIDI KUTIKISA AFRIKA...