Home Uncategorized YANGA YAPINDUA MEZA USAJILI WA GADIEL

YANGA YAPINDUA MEZA USAJILI WA GADIEL


MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msolla amezungumzia mjadala wa usajili wa beki wa pembeni, Gadiel Michael na kutoa ruhusa ya mchezaji huyo kwenda popote atakapohitaji ikiwemo Simba inayotajwa kuwa mbioni kumsajili lakini beki huyo ni kama amepindua meza kibabe.

Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku moja tangu Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwazuia mabosi wake kuendelea kumbembeleza beki huyo aliyegoma mara mbili kusaini mkataba mpya wa kubaki Yanga.

Wakati Zahera na Msolla wakitoa kauli hizo, upande wa Gadiel naye alitua jana jijini Dar akitokea Misri alikokuwa na majukumu ya timu ya taifa na kufunguka kuhusu hatima yake katika mahojiano maalum na gazeti hili akionekana kuiweka Simba kapuni kwa muda.

Yanga na Gadiel Mara ya mwisho ni wiki iliyopita, Yanga kupitia mmoja wa mabosi wa klabu hiyo, alipanda ndege na kumpelekea mchezaji huyo mkataba akasaini akiwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kinashiriki Afcon nchini Misri.

Msolla ameliambia Championi Ijumaa kuwa, suala hilo lipo kwake hivi sasa na ataamua yeye asaini au asisaini, lakini kwao viongozi wamelifunga suala hilo.

Msolla alisema kuwa, hatasikitika kuondoka kwa beki huyo lakini atashangazwa na maamuzi yake atakayoyachukua ya kuchelewa kuwapa taarifa viongozi wa timu hiyo tangu awali kuwa anaondoka na badala yake kutafuta mchezaji mwenye hadhi na kiwango kikubwa cha kuichezea Yanga.

SOMA NA HII  JEZI YA TAMBWE KUWA NA UKAME WA MABAO YANGA LAMFANYA ATOE TAMKO KWA URIKHOB