Home Uncategorized KMC YAPANIA KUFANYA KWELI RWANDA

KMC YAPANIA KUFANYA KWELI RWANDA

UONGOZI wa KMC umesema kuwa utaitumia michuano ya kombe la Kagame kwa ajili ya kujiaandaa na michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa kwa sasa kikosi kimeweka kambi nchini Rwanda kwa ajili ya michuano ya Kagame ambayo inaanza kutimua vumbi kesho.

“Tupo sawa na tumejipanga kufanya maajabu kwenye michuano hii, tunatambua mashabiki wanatuombea nasi tutafanya kweli hatutawaangusha, kwani tutatumia michuano hii kwa ajili ya kujiaanda na michuano ya kimataifa ikiwa ni kombe la Shirikisho pamoja na mashindano ya Ligi Kuu Bara,” amesema.

SOMA NA HII  KATI YA MORRISON, TUNOMBE,KISINDA,SARPONG, HUYU HAPA AMEWAPOTEZA WOTE