Home Uncategorized PRESHA YA MENEJA MPYA WA CHELSEA LAMPARD IPO NAMNA HII

PRESHA YA MENEJA MPYA WA CHELSEA LAMPARD IPO NAMNA HII

MENEJA mpya wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa anatambua presha kubwa ya bosi wa kikosi hicho, Roman Abramovich hasa timu inaposhindwa kupata matokeo chanya.

Lampard ameajiriwa na Chelsea kwa kandarasi ya miaka mitatu akibeba mikoba ya Maurizo Sarri ambaye ametimkia Juventus.

Mpaka sasa Abramovich amefanya kazi na makocha 13 tangu ainunue klabu hiyo mwaka 2003.

“Nikiwa mchezaji nakumbuka vizuri wakati Abramovich alipotua kwenye klabu alitusisitiza kwamba anapenda kuona mafanikio makubwa kisoka, hivyo najua nina kazi ngumu ya kufanya,” amesema Lampard ambaye ametoka kikosi cha Derby Country.

SOMA NA HII  UWEZO WA KAPOMBE WAMVUTIA BEKI HUYU ANAYEKIPIGA KCB, ATAKA KUJA SIMBA