Home Simba SC UONGOZI SIMBA WAFUNGUKIA ISHU YA KAGERE KUTOCHEZA

UONGOZI SIMBA WAFUNGUKIA ISHU YA KAGERE KUTOCHEZA


 OFISA Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa hakuna anayeweza kumpangia majukumu Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes katika utendaji wake wa kazi.

Hayo ameyasema ikiwa ni baada ya kuenea kwa taarifa kwamba wakala wa mchezaji wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba kudai kuwa mteja wake hapewi nafasi kikosi cha kwanza kucheza.

Msimu huu wa 2020/21 maisha ya Kagere kikosi cha kwanza yamekuwa ni ya kuunganisha licha ya kwamba ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 11.

Gomes amekuwa akipenda kumtumia Chris Mugalu na wakati mwingine kutumia viungo katika kufanya mashambulizi.

Manara amesema:”Nimeona kwamba kwenye mitandao ya kijamii inaeneza taarifa kuhusu wakala wa Kagere akidai kwamba mchezaji wake hachezi hilo sio sawa na hakuna ambaye anayeweza kumpangia majukumu kocha.

“Ikiwa ni wakala wa mchezaji basi anapaswa apambane kuhusu stahiki za mteja wake labda ingekuwa sawa ila kuhusu kupewa nafasi ya kuanza ma kutoanza hilo ni jukumu la kocha,”.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA KUSEPA SIMBA....MGUNDA ATAJA GONGWA LINALIMTESA OKWA...