Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA KUSEPA SIMBA….MGUNDA ATAJA GONGWA LINALIMTESA OKWA…

SIKU CHACHE BAADA KUSEPA SIMBA….MGUNDA ATAJA GONGWA LINALIMTESA OKWA…

Habari za Simba

Nyota Nelson Okwa ambaye ni mali ya Simba kaibuka ndani ya kikosi cha Ihefu chenye maskani yake Mbeya, nyanda za juu Kusini.Hakuwa na msimu mzuri ndani ya Simba ingizo hilo jipya kutokana na kushindwa kuonyesha makeke uwanjani.

Sababu kubwa ya kukwama kufanya vizuri ni kusumbuliwa na majeraha ambapo alitumia muda mwingi kupambania hali yake kabla ya kuanza kurejea mdogomdogo.

kwa mujibu wa Juma Mgunda ambaye ni kocha msaidizi wa Simba, hivi karibuni aliweka wazi kuwa sababu kubwa ya Okwa kutoonekana uwanjani ni kusmbuliwa na nyonga.

“Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa Okwa hayupo fiti na anasumbuliwa na nyonga hivyo anapambania hali yake akitengamaa atarejea uwanjani,”.

Akiwa na Simba kwenye mechi za ligi ni mbili alicheza na kuyeyusha dakika 13 hakupata nafasi ya kufunga wala kutengeneza nafasi ya bao.

Mwingine ambaye yupo ndani ya Ihefu ni Victor Ackpan ambaye alikuwa akicheza pamoja na Okwa wapo hapo kwa mkopo.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AWAPIGA MKWARA MASTAA WANAOCHEZA 'KIFAZA FAZA' SIMBA...