Home Habari za michezo HI HAPA SIRI YA BALEKE WA SIMBA…KUTIKISA NYAVU LIGI YA MABINGWA…AMEZUNGUMZA HAYA

HI HAPA SIRI YA BALEKE WA SIMBA…KUTIKISA NYAVU LIGI YA MABINGWA…AMEZUNGUMZA HAYA

Habari za Simba SC

STRAIKA wa Simba, Jean Baleke anaitazama Ligi ya Mabingwa Afrika, namna inavyoweza kuongeza maarifa zaidi kwa wachezaji wenye mitazamo ya kufika mbali kwenye karia yao.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Baleke alisema kwenye michuano hiyo wanakutana na wachezaji wenye uwezo tofauti, hivyo kuna vitu vya kujifunza na kuvifanyia kazi katika majukumu yao ya kila siku, kuhakikisha wawapo uwanjani wanakuwa na vitu vipya vyenye manufaa kwa timu yao.

Beleke ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi dhidi ya Raja Casablanca, Simba ikipoteza mabao 3-1 mechi ya kukamilisha hatua ya makundi.

Beleke alisema anaamini katika kujifunza maarifa mapya zinapotokea fursa kama za michuano ya CAF akiamini kazi yake inahitaji mbinu na ubunifu kila mara.

“Kwenye michuano ya CAF tunakutana na wachezaji wenye viwango tofauti, wanacheza ligi tofauti yapo ya kujifunza kwao, na wao yapo ya kujifunza kwetu, mchezaji anayeipenda kazi yake hachoki kupata vitu vipya kwenye kichwa chake.

“Binafsi nimejifunza vingi kwanza kujiamini kunaongezeka, kutamani kufanya vitu vikubwa zaidi, mengine ni siri yangu yataonekana uwanjani wakati wa kuisaidia timu yangu kwenye michuano mbalimbali.”

Staa huyo amefunga mabao matano kwenye Ligi Kuu alifunga dhidi ya Dodoma Jiji, Singida Big Stars na hat-trick dhidi ya Mtibwa Sugar, kwa upande wa CAF ana mabao matatu.

“Kufunga ni jukumu langu kila ninapopata nafasi ya kufanya hivyo, maana yangu ni kwamba tunacheza watu wengi uwanjani nikiona mchezaji mwenzangu yupo nafasi ya kufunga natoa pasi, wote tunajenga Simba moja;

“Mbele yetu tuna kazi nyingi tunapaswa kuelekeza nguvu kupambana kwa pamoja ili tufanikiwe kwa pamoja, mfano baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya CAF tunapaswa kuongeza ushindani zaidi ili tufanikiwe.”

SOMA NA HII  HUYU HAPA REFA ATAKAYECHEZESHA MECHI YA YANGA...KUMBE ALICHEZESHA MECHI YA PSG NA INTER