Home Habari za michezo KISA USAJILIWA BALEKE….MOSES PHIRI AANIKA WASIWASI WAKE SIMBA…AFUNGUKA A-Z…

KISA USAJILIWA BALEKE….MOSES PHIRI AANIKA WASIWASI WAKE SIMBA…AFUNGUKA A-Z…

Habari za Simba

Mshambuliaji wa Simba SC, Moses Phiri hana wasiwasi na usajili mpya uliofanywa na timu hiyo hasa kugombea nafasi ya kucheza na kwamba kwa upande wake yuko tayari kushindana nao labda kwa upande wao.

Phiri ametoa kauli hiyo jana alipowasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea Dubai ambako Simba iliweka kambi ya siku kadhaa.

Kinara huyo wa mabao kwa Simba ameeleza kuwa wachezaji hao wataongeza thamani kubwa kwenye kikosi hicho, na kwamba kwenye timu yoyote lazima kuwe na wachezaji wengi ili kutoa nafasi ya wengine kusubiri kutokana na chaguo la kocha.

“Mimi niko tayari kushindana nao, sijawahi kucheza nao ila nina uhakika ni wachezaji wazuri wataongeza kitu kwenye timu,”amesema Phiri.

Simba ina washambuliaji wanne, Habib Kyombo, John Bocco, Jean Baleke, na Moses Phiri.

SOMA NA HII  RAIS "HAKUNA WA KUIZUIA YANGA KUTWAA UBINGWA CAF...AMEFUNGUKA HAYA