Home Habari za michezo RAIS “HAKUNA WA KUIZUIA YANGA KUTWAA UBINGWA CAF…AMEFUNGUKA HAYA

RAIS “HAKUNA WA KUIZUIA YANGA KUTWAA UBINGWA CAF…AMEFUNGUKA HAYA

River vs Yanga SC

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa hakuna timu ya kuizuia Yanga kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwani timu hiyo ina benchi bora la ufundi na wachezaji wenye ubora ambao wanaweza kufanya jambo hilo.

Kauli hiyo ya Hersi inakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya kuibuyka na ushindi wa bao 2-0 katika mchezo wao wa kwanza robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Rivers United uliopigwa jana Jumapili nchini Nigeria.

“Sisi ni wadogo, tumeikuta hii klabu, na maleng yetu ni kuchukua ubingwa kwenye mashindano yoyote tunayoshiriki. Sishangai kuona malengo yetu kwenye mashindano ya kimataifa yanaanza kukomaa.

“Yanga haikuwa kwenye nafasi nzuri katika mashindano ya kimataifa, lakini sasa imethubutu na tumefika makundi na kumaliza nafasi ya kwanza, baada ya hapo tukaingia robo fainali, leo tumeshinda mchezo wetu wa kwanza ugenini, tuna faida ya bao 2 na mechi ijayo tutakuwa nyumbani.

“Njia ya nusu fainali tunaiona ni nyeupe, ukivuka huko chochote kinaweza kutokea, kwa nini isiwe Yanga ikapata nafasi ya kuchukua ubingwa huu wa Kombe la Shirikisho Afrika? Itakuwa furaha kwa mashabiki, viongozi na Tanzania kwa ujumla.

“Inawezekana tukiweka focus yetu kama viongozi, benchi la ufundi na wachezaji. Mechi ya dabi tulipoteza lakini sisi kama viongozi tuna wajibu wa kuilinda timu isiathirike na maneno nje ya uwanja.

“Kutibu kidonda na kufocus kwenye kile ambacho tumekipanga, na hilo ni kuingia nusu fainali, fainali na kuchukua ubingwa, kwani kuna ubaya gani?

“Fainali ya mwaka huu ni mfumo wa nyumbani na ugenini, kwa hiyo utakuwa na faida ya kucheza nyumbani kwako na ugenini, kwa hiyo tukichanga karata vizuri tunaweza kufikia malengo,” amesema Eng. Hersi.

SOMA NA HII  KENO BONANZA SIRI YA MAFANIKIO YA MCHEZO YA KUBASHIRI ILIYOFICHULIWA