Home Habari za michezo KUBALI AU KATAA…ILA KITAKWIMU…NTIBAZONKIZA KAZIDIWA NA MAYELE TU YANGA NZIMA..

KUBALI AU KATAA…ILA KITAKWIMU…NTIBAZONKIZA KAZIDIWA NA MAYELE TU YANGA NZIMA..

Habari za Simba

Saidoo Ntibazonkiza sasa amefunga mabao matano katika dakika 184 alizocheza kwenye NBC Primia Ligi akiwa na Simba SC, mabao hayo ni mengi zaidi ya manne aliyoyafunga katika dakika 1025 alizocheza akiwa na Geita Gold.

Saidoo Ntibazonkiza katika Nbc premier league msimu huu akiwa na Geita Gold

michezo 14

dakika 1025

mabao 4

Saidoo Ntibazonkiza katika NBC Primia Ligi msimu huu akiwa na Simba Sc

michezo 2

dakika 184

mabao 5

Saidoo Ntibazonkiza pia sasa ndiye mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi msimu huu kwenye NBC Primia Ligi, mabao (17) sawa na Fiston Mayele.

Saidoo Ntibazonkiza (17)

Fiston Mayele (17)

Cloutus Chama (15)

Sixtus Sabilo (13)

Moses Phiri (12)

John Bocco (10)

Takwimu za Ntibazonkiza kwenye Nbc premier league msimu huu, kwa na Geita Gold pamoja na Simba Sc.

michezo 14

dakika 1205

mabao 9

pasi za mabao 8

amehusika katika mabao 17

Ana wastani wa kufunga bao au kutoa pasi ya bao kila baada ya dakika 70.

Kwa kasi aliyonayo Saido kwa sasa ni dhahiri kuwa amekuwa tishio kwa Mshambuliaji wa Yanga Fiston Kalala Mayele.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI