Home Simba SC USHINDI MBELE YA AS VITA NA BIASHARA UNITED WAIPA NGUVU SIMBA

USHINDI MBELE YA AS VITA NA BIASHARA UNITED WAIPA NGUVU SIMBA


KOCHA Mkuu wa Simba anayefanya kazi kwa ukaribu na Seleman Matola ambaye ni msaidizi wake amesema kuwa wamekubaliana kupambana kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Simba itashuka Uwanja wa Mkapa, Februari 23 kusaka pointi tatu mbele ya Al Ahly wakiwa na sera ya Total War, A Point Of No Return wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi zama zile za Patrick Aussems waliposhinda bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.

Tayari kikosi hicho kimeanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.

Gomes amesema kuwa kundi A lina ushindani mkubwa na ushindi wao mbele ya AS Vita wa bao 1-0 umeongeza nguvu kwao ya kupambana pamoja na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Raia huyu wa Ufaransa ambaye ni mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga ndani ya Simba Januari 7 amesema kuwa wapo tayari na wanawaheshimu wapinzani wao.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari na tunawaheshimu wapinzani wetu, kikubwa ni kwamba tutaingia ndani ya uwanja kwa tahadhari.

“Ushindi wetu mbele ya AS Vita umeongeza nguvu na morali kwa wachezaji kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya vizuri hivyo imani ni kwamba tutapambana na kupata matokeo chanya,” . 

SOMA NA HII  FT: SIMBA SC 4-0 PAMBA FC....MHILU AONA MWEZI LEO....KIBU MWENDO WA KIMYA...SIMBA WAIFUATA YANGA KIBABE..