Home news KUHUSU ISHU YA MGOGORO KATI YA PABLO NA WENZAKE…SIMBA WATOA TAMKO..ISHU NZIMA...

KUHUSU ISHU YA MGOGORO KATI YA PABLO NA WENZAKE…SIMBA WATOA TAMKO..ISHU NZIMA IKO HIVI…


MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, amesema licha ya timu yao kukosa matokeo mazuri katika michezo mitatu iliyopita ya Ligi Kuu Bara, lakini bado wapo imara na hakuna mgogoro wowote unaoendelea klabuni hapo, kila kitu ni shwari.

Kwenye mechi hizo tatu, Simba imepoteza mbili dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar, huku ikitoka suluhu na Mtibwa Sugar. Juzi Jumapili ilishinda 6-0 dhidi ya Dar City kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports hatua ya 32 bora.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mangungu alisema: “Hakuna mgogoro wowote baina ya benchi la ufundi na wachezaji wala bodi, naweza kukiri hayo yanayosemwa ni propaganda za watu wa mataani tu.

SOMA NA HII  MASTAA WALIOTAJWA KUTUA SIMBA NA YANGA KWA MBWEMBWEEE...KUMBE UKWELI UKO HIVI....