Home news WAKATI AMANI IKIZIDI KUTAWALA KLABUNI…NABI AVUNJA UKIMYA YANGA…ADAI HAIWEZI KUWA RAHISI…

WAKATI AMANI IKIZIDI KUTAWALA KLABUNI…NABI AVUNJA UKIMYA YANGA…ADAI HAIWEZI KUWA RAHISI…


KOCHA Mkuu wa vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Nasreddine Nabi, ameweka wazi kuwa anaamini kama kikosi chake kitaendelea na kasi ambayo wanaenda nayo kwa sasa, basi ni wazi hakuna timu inayoweza kuwazuia katika malengo yao ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Yanga juzi Jumamosi wakiwa katika Uwanjawa CCM Kirumba jijini Mwanza, walifanikiwa kushinda 1-0 dhidi ya Mbao katika mchezo wa hatua ya 32 ya ASFC. Ushindi huo umewafanya wakate tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Tayari msimu huu Yanga wamefanikiwa kushinda taji la Ngao ya Jamii na mpaka sasa wao ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara na poiti zao 35, walizokusanya kwenye michezo 13.

Akizungumza hivi karibuni kocha Nabi alisema: “Tulitarajia kukutana na mchezo mgumu dhidi ya Mbao kama ambavyo ilitokea hasa kutokana na ukweli kuwa tulicheza na mpinzani ambaye hatakuwa tunamfahamu kiundani zaidi, lakini jambo zuri ni kwamba tulifanikiwa kuibuka na ushindi ambao umetupeleka hatua ya 16 bora.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ubingwa katika michuano yote ambayo tumesalia na tunashiriki msimu huu, tunajua haiwezi kuwa rahisi lakini tunaamini kuwa kama tutaendelea kucheza katika kasi hii basi hakuna wa kutuzuia.”

SOMA NA HII  ZA NDAANII....ISHU YA CHAMA KUTOLEWA JANA ...KUMBE MCHEZO MZIMA UKO HIVI...