Home Habari za michezo ZA NDAANII….ISHU YA CHAMA KUTOLEWA JANA …KUMBE MCHEZO MZIMA UKO HIVI…

ZA NDAANII….ISHU YA CHAMA KUTOLEWA JANA …KUMBE MCHEZO MZIMA UKO HIVI…

Habari za Simba

Nimeona mijadalaa wengi wakimlaumu kocha Robertinho juu ya uamuzi wa kumtoa Clatous Chama mapema sana mchezoni.

Nimekumbuka simulizi ya kisa cha Thierry Henry na Pep Guardiola katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya kati ya Barcelona na Sporting Lisbon.

Barcelona wakiwa wanacheza mpira mwingi sana, Henry aliamua kukiuka maelekezo ya Pep na kuacha eneo lake alilopangwa na kuhamia upande mwingine wa uwanja.

Muda mchache tu baada ya kuhama aliwapatia Barcelona bao la kuongoza na yeye mwenyewe alihisi kama alikuwa na mchezo mzuri.

Baada ya kuendelea kucheza kwa jinsi alivoona yeye mwenyewe ni sawa, Pep alimtoa na kumuelekeza kwamba alikuwa anavuruga plan yake.

Sub yake ilifanyika dakika ya 45 ya mchezo na kumbuka TH14 alikuwa mshambuliaji kinara na staa wa Barca.

Henry akamalizia kwamba Guardiola akiwa na plan unapaswa kuisimamia mpaka mwisho.

Nimefikiria sababu gani inaweza kumfanya kocha amuondoe Chama uwanjani mapema dakika ya 32 timu ikiwa inasaka matokeo. Kama si sababu tofauti na injury basi huenda Chama hakutii mpango wa kocha.

Makocha wote wakubwa duniani wanataka mchezaji aheshimu mpango wake. Kama watapoteza basi kocha ataulizwa.

Robetinho ameonesha mamlaka! Na inapaswa kuwa hivyo siku zote. Mpango wa kocha unapaswa kuheshimiwa.

SOMA NA HII  YANGA CHINI YA MATAJIRI ...MAMBO MAKUBWA YAJA..SENZO AFUNGUKA A-Z...