Home Habari za michezo BAADA YA KUTUA ZAKE IHEFU…OKWA ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA HAYA MAPYA YA SIMBA….

BAADA YA KUTUA ZAKE IHEFU…OKWA ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA HAYA MAPYA YA SIMBA….

Habari za Simba

Kiungo Nelson Okwa atakayeanza kucheza Ihefu kwa mkopo akitokea Simba, amesema yupo tayari kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha anarejea kwenye makali yake yatakayompa thamani kubwa.

Okwa ambaye tangu msimu huu uanze amecheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara ndani ya kikosi cha Simba, alisema anachokiamini ni kupata nafasi itakayomfanya kipaji chake kiweze kuonekana kwa ukubwa.

Okwa ilishindwa kupenya katika ya washindani wake wa namba ndani ya Simba ambao ni Ousmane Sakho, Clatous Chama, Moses Phiri na Mzamiru Yassin na ameongezeka Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ambaye mechi yake ya kwanza dhidi ya Prisons alifunga hat-trick na kutoa asisti timu yake ikishinda mabao 7-1 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Ndani ya kikosi cha Ihefu, Okwa anakwenda kukutana na Jafari Daud, Never Tigere na Papy Tshishimbi wanaocheza nafasi yake, hivyo atatakiwa kwenda kupambana zaidi kama anavyokiri mwenyewe.

Akizungumza  Okwa alisema; “Japokuwa timu zimetofautiana mipango, uchumi na mazingira, lakini hakuna mechi nyepesi mkiwa uwanjani kila timu inaingiza wachezaji 11 ili kushindana, ndio maana nasema nitakwenda kupambana.

“Nakwenda Ihefu kusaka changamoto mpya, mtazamo wangu ni kucheza na siyo vingine na kwa sasa siwezi kusema mambo mengi nasubiri nianze kazi ama kazi yangu ndio iongee zaidi.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA MAFANIKO YOOTE WALIYONAYO...HIVI NDIVYO YANGA INAVYOZIDI KUIKIMBIZA SIMBA...