Home Uncategorized DEMBELE YEYE ANAPIGA MAZOEZI TU

DEMBELE YEYE ANAPIGA MAZOEZI TU



NYOTA wa Barcelona, Ousmane Dembele amelazimika kufanya mazoezi peke yake baada ya mapumziko ya muda wa siku nne kwa timu yake ya Barcelona kutokana na uwepo wa mechi za kimataifa kwa timu za taifa.

Kikosi cha Barcelona kinachonolewa na Ronald Koeman kilipewa muda wa siku nne kwa ajili ya mapumziko kabla ya masuala ya ligi kurejea ili wachezaji walioitwa timu zao za taifa kutimiza majukumu yake.

Licha ya kwamba wachezaji wamepewa mapumziko, Dembele alirejea uwanjani na kuanza kufanya mazoezi peke yake. Baada ya dirisha la usajili kufungwa na dili lake la kuondoka ndani ya kikosi hicho kushindikana ameanza kujiweka sawa ili kurejea kwenye ubora.

Dembele alikuwa kwenye mpango wa kufanyiwa mabadilisho ili aweze kupata timu nyingine ila ilishindikana na amekuwa akishindwa kuonyesha makeke ndani ya kikosi hicho kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Winga huyo hajawa kwenye kikosi cha kwanza tangu Novemba ndani ya Barcelona kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

SOMA NA HII  UCHEBE AMPOTEZA JUMLAJUMLA SVEN NDANI YA SIMBA