Home Habari za michezo UNAAMBWA KUMBE SIRI YA MO DEWJI KUMTEUA TENA TRY AGAIN KUWA ‘BOSI...

UNAAMBWA KUMBE SIRI YA MO DEWJI KUMTEUA TENA TRY AGAIN KUWA ‘BOSI KAZI’ SIMBA NI HII…

Habari za Simba SC

Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji, amemteua kwa mara nyingine Salim Abdallah ‘Try Again’, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wekundu wa Msimbazi hao.

Dewji amefanya uteuzi huo katika hafla fupi ya kuwaaga wajumbe waliomaliza muda wao akiwamo Kassim Dewji, Mwina Kaduguda na Hussein Kita.

Mohamed Dewji, alisema kuwa anaimani na Try Again’ ndio maana amempa nafasi nyingine na anaamini ataendelea kuiongoza Simba kufikia mafanikio makubwa barani Afrika.

“Umefanya kazi nzuri ninaimani na wewe, nategemea utaifikisha Simba kwenye mafanikio makubwa ya soka barani Afrika na duniani kwa ujumla, ” alisema Mo Dewji.

Kwa upande wa Try Again, alisema anafurahi kuwa sehemu ya uongozi katika bodi hiyo na kwamba atahakikisha anaendelea kuitendea haki nafasi aliyopewa kwa mara nyingine kuifanya Simba kuwa imara.

“Asante sana ndugu Mo Dewji kwa imani yako juu yangu, nakuahidi utendaji bora kwenye nafasi hii ili kwa pamoja tunaweza kuifikisha Simba kwenye mafanikio makubwa ambayo inastahili,” alisema Try Again.

Mo Dewji alitumia hafla hiyo kuwapa vyeti wajumbe watatu ambao ni Murtaza Mangungu, Haroub Seleman na Asha Baraka ambao bado wako katika bodi hiyo wakipita kwa upande wa wanachama baada ya kuchaguliwa hivi karibuni.

Mo Dewji alimteua Try Again kuchukua nafasi yake Septemba mwaka 2021, baada ya kubanwa na shughuli zake za biashara ambapo amefanya kazi nzuri kabla ya kumteua tena kuongoza bodi hiyo.

SOMA NA HII  GOMES AFUNGUKA HAYA KUHUSU MAENDELEO YA MANULA