Home Simba SC GOMES AFUNGUKA HAYA KUHUSU MAENDELEO YA MANULA

GOMES AFUNGUKA HAYA KUHUSU MAENDELEO YA MANULA

Kocha Mkuu wa Simba SC, Didier Gomes amesema kuwa Hali ya afya ya Golikipa wake namba Moja Aishi Manula si mbaya.

Gomes, amesema hayo mara baada ya mchezo wa ligi kuu baina ya Simba SC na JKT Tanzania kumalizika ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa goli 3-0 huku Aishi Manula alishindwa kuendelea na mchezo mara baada ya kuumia na kukimbizwa Hospitali.
Gomes amesema kuwa kwa Sasa anangojea taarifa ya Daktari wa timu Ili kujua ni kiasi gani Golikipa huyo ambaye pia ni Golikipa namba Moja wa timu ya Taifa ,Taifa Stars ameumia.
“Baada ya mchezo kuisha daktari ameniambia kuwa kila kitu kipo sawa, amepelekwa hospitali kufanyiwa vipimo na tunasubiri majibu. Manula ni mchezaji muhimu sana na nina uhakika ataweza kucheza Sudan.”-
SOMA NA HII  MANZOKI HUYU HAPA....AFUNGUKA SIKU YA KUJIUNGA SIMBA...IPACHIKA JINA JIPYA YANGA...