Home Simba SC SIMBA YASEPA NA POINTI TATU MAZIMA ZA JKT TANZANIA KWA MKAPA,BOCCO,MUGALU WATUPIA

SIMBA YASEPA NA POINTI TATU MAZIMA ZA JKT TANZANIA KWA MKAPA,BOCCO,MUGALU WATUPIA

 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, leo Machi Mosi kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania.


Mchezo huu wa leo ni wa 19 kwa Simba ikiwa ina mechi mbili mkononi ili kuweza kuwafikia vinara wa ligi ambao ni Yanga wakiwa wamecheza jumla ya mechi 21.

Mabao ya Simba yalifungwa na Chris Mugalu dakika ya 9 lile la pili lilifungwa na Luis Miquissone dakika ya 38 na kuwafanya mabingwa hao watetezi kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao hayo mawili.

Kipindi cha pili JKT Tanzania waliweza kuleta ushindani wakitaka kumtungua Beno Kakolanya ambaye alichukua nafasi ya Aishi Manula ambaye alipata majeraha na kupelekwa hospitali kwa huduma zaidi.

Licha ya jitihada hizo ngome ilikuwa ngumu kwa Simba chini ya Pascal Wawa aliyekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Kenedy Juma, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Tshabalala kwenye eneo la ulinzi.

Msumari wa tatu ulipachikwa na John Bocco dakika ya 90+3 kwa pasi ya Rarry Bwalya. 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 45 kibindoni ikiwa nafasi ya pili huku vinara wakiwa na pointi 49.

SOMA NA HII  KISA MECHI YA SIMBA vs YANGA....VAR KUANZA KUTUMIKA KWENYE MECHI ZA LIGI KUU BONGO...