Home Uncategorized KUWAONA VINARA WA LIGI WAKIKIPIGA DHIDI YA MAFUNZO BUKU MBILI

KUWAONA VINARA WA LIGI WAKIKIPIGA DHIDI YA MAFUNZO BUKU MBILI

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC leo Oktoba 10 wana kibarua cha kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex. Kiingilio kwa mzunguko leo ni 2,000 (buku mbili).


Kushuhudia burudani kwenye mchezo huo ni kwa viingilio vya bei poa kabisa vya Kitanzania, cha chini kikiwa Sh. 2,000 (Mzunguko), Sh. 3,000 (V.I.P B) na Sh. 5,000 (V.I.P).

Azam FC inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Oktoba 15 Uwanja wa Azam Complex.


Ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi tano za ligi na imeshinda mechi zote.

Kwa Septemba imetoa mchezaji bora ambaye ni Prince Dube na kocha bora ambaye ni Aristica Cioaba.
SOMA NA HII  MAKAMBO ATOA AHADI YA KUWAJAZA MASHABIKI AKIFUNGA MBELE YA SIMBA