Home news BAADA YA KUISULUBU ASEC…SIMBA WAPEWA MCHONGO MPYA CAF…TYR AGAIN AITAJA SUPER CUP….

BAADA YA KUISULUBU ASEC…SIMBA WAPEWA MCHONGO MPYA CAF…TYR AGAIN AITAJA SUPER CUP….


NI mwanzo mzuri kwa Simba, kupata pointi tatu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf), kumewaibua wachezaji wa timu nyingine kuwapa mbinu za kushinda ugenini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kwanza anawashukuru mashabiki wa Simba kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani na waendelee kusherekea.

Alisema wanachohitaji zaidi ni umoja zaidi kwani wamepania kufanya mambo makubwa kwenye michuano hiyo ya kimataifa msimu huu na si lazima kila silaha wanayotumia waiweke wazi kwa maadui zao kwani wanajua na wana uzoefu mkubwa na timu za Afrika. Anasema sababu kubwa ya kushinda mechi ya juzi ni mshikamano baina yao na wamejipanga vizuri kila hatua ya wanayokanyaga ndio maana amewataka mashabiki kuwaombe na kuwapa sapoti kubwa iliyoko ndani ya uwezo wao kila wanapocheza.

Alisema wanaendelee kupambana kwani Simba ni timu kubwa na wanajua kucheza mechi kama hizo za kimataifa na kila mmoja ameona kilichotokea kwa Asec Mimosas.

“Tulizungumza na wachezaji na tuliweka mipango ya mpira na ukweli katika eneo hilo Simba tupo vizuri, tuna utulivu wa kutosha na tunatambua nini tunafanya,” alisema Try Again na kuongeza;

“Tulikaa na wachezaji wetu, tulikaa na benchi la ufundi tulijua Mimosas ni timu ngumu na haifungiki kirahisi na tunajua historia yao hawajapoteza mechi na tulifanya kile kinachostahili kufanyika hatimaye tumepata matokeo mazuri,”

“Siri ya Simba kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa maana yake ni mcheza kwao hutunzwa hakuna zaidi ya hapo. Mipango yetu katika mechi zijazo niweke wazi na watu wote wafahamu haya mashindano ya kimataifa ndio mashindano yetu, ndio levo yetu na nafikiri wametangaza mashindano ya (Super Cup) na tutakwenda kucheza huko na sisi ni timu kubwa tupo tayari kwa hilo.

“Yote kwa yote niwambie Wanasimba tumejipanga na tunajua tunachokifanya na tuna mipango mizuri na kuhakikisha tunapasua katika mashindano haya ya kimataifa kwani haya kwetu ni mashindano ya kawaida.”

Katika hatua nyingine bosi huyo alisema hata mechi ijayo dhidi ya USGN ya Niger inayotarajiwa kucheza Februari 20 Jumapili, watafanya vizuri huku wachezaji pia wakishauriwa cha kufanya na wakongwe mbalimbali.

SOMA NA HII  MAMA SAMIA AAPISHWA KUWA RAIS WA TANZANIA – VIDEO

Kipa wa Ruvu Shooting, Mohamed Makaka alikiri Simba kuwa nzuri michuano ya Caf, pamoja na hilo alishauri mastaa kuusoma mchezo unataka nini na kuongeza umakini hadi kipenga cha mwisho (dakika 90).

“Simba ina uzoefu mkubwa na michuano hiyo, ninachoweza kuwashauri mastaa wa timu hiyo, kila mmoja akafanye kazi yake kikamilifu, naamini watafanikiwa zaidi na ndio wanaoiwakilisha nchi kwa sasa,” alisema Makaka na kuongeza;

“Wakipata bao la kuongoza wajitahidi kulilinda na kutoridhika wakijua wapinzani wao wapo kwa ajili ya kutaka ushindi, safu ya mbele mmoja akikabwa sana wengine watumie nafasi hiyo kufunga.

Wakati Kipa wa Mbeya City, Deogratius Munishi ‘Dida’ alisema kuwa; “Ujue wasiichukulie Simba kufungwa mechi mbili na sare sare nne haimanishi wana timu mbaya ni upepo tu ndio maana mechi ya juzi wamewafunga wapinzani wao.”

Simba msimu huu imepania kucheza nusu fainali ya Shirikisho Afrika ikiwa ni hatua kubwa zaidi kwao kwenye mashindano hayo yenye fedha nyingi Afrika. Try Again ameweka wazi malengo yao waliyompa Kocha ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA pamoja na kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika. Simba ipo kundi moja na timu za RS Berkane ya Morocco, USGN ya Niger pamoja na Asec ya Ivory Coast ambayo mpaka jana mchana bado ilikuwa Jijini Dar es Salaam haijarudi kwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here