Home Uncategorized MAKAMBO ATOA AHADI YA KUWAJAZA MASHABIKI AKIFUNGA MBELE YA SIMBA

MAKAMBO ATOA AHADI YA KUWAJAZA MASHABIKI AKIFUNGA MBELE YA SIMBA


 KUELEKEA mechi dhidi ya Simba, mshambuliaji wa Yanga, Heritier Ebenezer Makambo, amefunguka kuwa mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kuja kwa wingi kuushuhudia mchezo huo huku akiweka wazi kuwajaza pindi atakapofanikiwa kuifunga Simba.

Yanga leo Jumamosi watakuwa na kibarua kizito cha kumenyana na Simba katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu msimu wa 2021/22 utakaochezwa, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 Makambo amesema kuwa wao kama wachezaji wameshajiandaa kwa ajili ya mchezo huo hivyo kilichobaki ni mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuwapa hamasa ya kufanikisha ushindi huo huku akiweka wazi kuwajaza mashabiki wa timu hiyo endapo atafanikiwa kuifunga Simba.


 “Tayari tumeshajiandaa kwa siku kadhaa kukabiliana na Simba katika mchezo wa fainali, kinachotakiwa kwa sasa ni mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kutupa nguvu na hamasa kuelekea katika mchezo huu ambapo kama nitafanikiwa kuwafunga Simba basi kama kawaida nitawajaza wana Yanga.


“Unajua ni ngumu kutoa ahadi ya kufunga bao kwa kuwa inawezekana kama mchezaji usiwepo katika mipango ya mwalimu lakini yote kwa yote hakuna mchezaji asiyependa kufunga au kufanya vizuri katika mechi muhimu kama hii,” alisema mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  WACHEZAJI SABA SIMBA KUACHWA - VIDEO