Home kimataifa CONTE AGOMA DILI LA ARSENAL NA BARCELONA

CONTE AGOMA DILI LA ARSENAL NA BARCELONA


KOCHA Antonio Conte hana mpango wa kujiunga na Barcelona ama Arsenal kwa muda huu kwa kuwa anataka kuanza na timu tangu mwanzo wa msimu.

Conte mwenye miaka 52 kwa sasa hana kazi baada ya kuvunja mkataba na Inter Milan kufuatia kuwaongoza kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Serie A baada ya kuyeyuka miaka 11.

Kama sehemu ya makubaliano ya kuvunja mkataba , Conte amezuiwa kujiunga na timu nyingine ya Seria A mpaka msimu mpya unaofuata na sio sasa.

Ripoti zimeeleza kuwa Conte alikuwa amewekwa kwenye rada za Barcelona na Arsenal ila amekacha madilo hayo na badala yake anataka kuanza na timu tangu mwanzo.

SOMA NA HII  POCHETTINO ATAJWA SPURS