Home Habari za michezo GEORGE MPOLE AWAPA NENO HILI WANAOMCHUKULIA POA….APANIA KUIBEBA DHAHABU YA JOHN BOCCO…

GEORGE MPOLE AWAPA NENO HILI WANAOMCHUKULIA POA….APANIA KUIBEBA DHAHABU YA JOHN BOCCO…


Straika wa Geita Gold, George Mpole juzi amefunga bao lake la 13 kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu na kuongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu huku akitoa neno kwa waliomchukulia poa.

Bao la dakika ya 11 alilolifunga dhidi ya Mbeya Kwanza likiipa Geita ushindi wa 1-0, limemfanya Mpole kupanda juu kwenye msimamo wa wafungaji bora kwa bao moja huku akifuatiwa na Fiston Mayele wa Yanga (12) ambaye hajafunga kwenye mechi nne mfululizo zilizopita.

Akizungumza Mpole alisema anaamini ataendelea kuwashangaza watu wengi ambao walikuwa hawana imani naye na kuweka wazi nia yake ya kutaka kiatu cha dhahabu.

“Namshukuru kocha wangu na benchi la ufundi la Geita kwa kuniamini. Nipo hapa kuipambania timu kuhakikisha inafikia malengo yake kisha ndio malengo yangu binafsi yanafuata,” alisema Mpole na kuongeza;

“Mwanzo hakuna aliyeamini kama nitafikisha mabao haya, wengi walinichukulia poa lakini nashukuru Mungu milango imefunguka.

“Nadhani hadi kufika mwisho wa msimu nitakuwa nimefunga zaidi na kuibuka mfungaji bora kwani ndio lengo langu na ndoto ya kila mshambuliaji.”

Mpole alifichua siri ya kasi yake ya kupachika mabao kuwa ni kujituma na ushirikiano bora alionao na wachezaji wenzake wa Geita.

“Kujituma, nidhamu na kufuata maelekezo ya makocha ndio silaha ya ushindi pia umoja na ushirikiano wa dhati kwa timu nzima yote hayo yamenifanya kuwa bora,” alisema.

Mpole alisajiliwa Geita mwanzoni mwa msimu huu akitokea Polisi Tanzania ambako aliachwa kwa kile kilichoelezwa kutoridhishwa na kiwango chake, lakini sasa kawa lulu.

SOMA NA HII  BAADA YA MANARA KUHUKUMIWA JANA....YANGA WASHINDWA KUJIZUIA...WATOA TAMKO ZITO....WAAPA KUCHUKUA HATUA...