Home Habari za michezo UWEZO WA KRAMO WAMUIBUA KIGOGO WA SIMBA….AFUNGUKA A-Z YANAYOENDELEA…

UWEZO WA KRAMO WAMUIBUA KIGOGO WA SIMBA….AFUNGUKA A-Z YANAYOENDELEA…

Habari za Simba

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, amesema nyota wao Aubin Kramo ana balaa akiwa kwenye uwanja wa mazoezi jambo linaloongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Nyota huyo aliyeibuka Simba msimu huu akitokea ASEC Mimosas, hajaonesha makeke yake uwanjani katika mechi za kimashindano kutokana na kusumbuliwa na majeraha, lakini kwa sasa yupo fiti.

Ally alisema wachezaji wote wapo tayari kwa mechi zilizopo mbele yao ikiwa ni zile za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na African Football League.

“Kramo hakuwa kwenye mechi ambazo timu ilicheza kwa sababu alikuwa bado hajawa fiti, lakini kwa sasa taratibu anazidi kuwa imara kutokana na kile ambacho anakionesha mazoezini ni balaa kubwa.

“Wale ambao walikuwa wanabeza uwezo wake watakutana naye uwanjani. Hakika kwenye mashindano yaliyopo mbele yetu wachezaji wapo tayari na burudani itaonekana kwa Wanasimba wote,” alisema Ally.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba inatarajia kucheza na Power Dynamos, ukiwa ni mchezo wa hatua ya kwanza wakianzia ugenini Septemba 16, huku African Football League wakipangwa dhidi ya Al Ahly, Oktoba 20, mwaka huu.

SOMA NA HII  KUHUSU KUMSAJILI BOBOSI...SIMBA SC WAPIGILIA MSUMARI....DILUNGA ATAJWA...