Home kimataifa ANAITWA KANTE, KIUNGO BORA DUNIANI

ANAITWA KANTE, KIUNGO BORA DUNIANI


 BONGE moja ya kiungo wa kati, mtibua mipango asiyechoka muda wote anatajwa kwa sasa kuwa miongoni mwa viungo bora duniani si mwingine anaitwa N’Golo Kate raia wa Ufaransa asiye na makuu awapo kazini.

Aliletwa duniani Machi 29,1991 ana umri wa miaka 30 na ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Chelsea kwa sasa Thomas Tuchel ambaye anakubali pia uwezo wake.

Urefu wake ni m 1.68, jezi anayoivaa ni namba 7 na ana uraia wa mataifa mawili ikiwa ni Ufaransa na Mali kwa sababu wazazi wake walikuwa ni wakimbizi kutoka Mali na waliibukia nchini Ufaransa mwaka 1980. Lakini kwa sasa nguvu kubwa ameiwekeza Ufaransa.

Kabatini ana tuzo moja ya mchezaji bora wa mwaka ambayo aliipata mwaka 2017 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, amenyanyua mara moja taji kubwa duniani ambalo ni Kombe la Dunia ilikuwa ni mwaka 2018 akiwa na timu ya Ufaransa.

Mara mbili ametwaa taji la Ligi Kuu England mwaka 2016 na 2017, taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa msimu wa 2020/21, taji moja la FA mwaka 2018, Europa League 2018/19 na taji moja la UEFA Super Cup msimu wa 2021/22 mataji yote haya akiwa na Chelsea.

Mkataba wake ndani ya Chelsea ambayo alijiunga nayo Julai 16,2016 akitokea Klabu ya Leicester City unatarajiwa kumeguka Juni 30,2023.

Rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya Chelsea amecheza jumla ya mechi 159 na kwa nafasi yake ya kiungo ametupia mabao 9 ni katika Ligi Kuu England huyu ni kiungo wa kazi, kazi zote ngumu huwa anapewa yeye na tabasamu lake kuliona akiwa uwanjani utasanda.

SOMA NA HII  KOCHA ARSENAL: OZIL ALICHANGANYIKIWA