Home epl MOURINHO ALIA NA VAR KISA KIWIKO CHA POGBA

MOURINHO ALIA NA VAR KISA KIWIKO CHA POGBA


KOCHA Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho anaamini kwamba kiungo wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi kutokana na kuonekana akimpiga kiwiko mchezaji wake Serge Aurier.


Mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Tottenham Hotspur, ubao ulisoma Tottenham 1-3 Manchester United. Pointi tatu hizo zinaifanya United kufikisha pointi 63 ikiwa nafasi ya pili na Tottenham pointi zake ni 49 nafasi ya 7.

Bao pakee la Tottenham lilipachikwa kimiani na Son Heung-min dakika ya 40 huku yale ya Manchester United yakifungwa na Fred dakika 57, Edinson Cavan dakika ya 79 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Mason Greenwood dakika ya 90+6.

Mourinho amesema kuwa kwa kitendo ambacho alikifanya Pogba VAR ilimlinda jambo ambalo liliwafanya wasiwe na bahati kwenye mchezo huo. 

“Maoni yangu ni kwamba tumepoteza mchezo ila haya matokeo hatukustahili kuyapata lakini tumepoteza mbele ya timu nzuri.

“Hatukuwa na bahati kwa sababu labda a Paul Pogba alipaswa kuonyeshwa kadi nyekundu ili atoke kwa sababu alimpiga kiwiko Serge Aurier. Labda tunaweza kwenda kuzungumza kuhusu VAR,” .

SOMA NA HII  LIVERPOOL KUKIWASHA NA MAN CITY NA MECHI KIBAO WIKIENDI HII