Home Yanga SC YANGA: LIGI YA TANZANIA NI NGUMU

YANGA: LIGI YA TANZANIA NI NGUMU

 


NAHODHA wa kikosi cha Yanga, Lamine Moro raia wa Ghana amesema kuwa ligi ya Tanzania ni ngumu kutokana na ushindani uliopo kwenye kila mechi ambayo amekuwa akicheza.


Lamine ni kinara wa utupiaji kwa mabeki wanaocheza ligi akiwa amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.

 Lamine amesema kuwa tangu anafika Tanzania ameona namna ligi ilivyo kuwa ngumu kwa wapinzani kuonyesha ushindani mkubwa.

“Tangu nimefika Tanzania sijawahi kuona mechi rahisi kwangu hasa kwa Yanga, ushindani huo umekuwa ukitufanya nasi tuzidi kuongeza juhudi ili kupata matokeo,” .

Mchezo wao uliopita mbele ya  KMC, Yanga ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 baada ya dakika 90 kukamilika, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya kwanza ina pointi 51 na KMC ipo nafasi ya 6 na pointi zake ni 36.

SOMA NA HII  MAYELE AFICHUA WALICHOWAFANYIA WACHEZAJI WA MAZEMBE WAKATI MECHI IKIENDELEA JANA...