Home Uncategorized MUUAJI WA SIMBA ATOA NENO LAKE LA MOYONI

MUUAJI WA SIMBA ATOA NENO LAKE LA MOYONI


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa alichokifanya mbele ya Simba ni sehemu ya kitu anachokipenda na imetokana na sapoti ya mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.

Morrison, jana Machi 8, Uwanja wa Taifa alizima kelele za mashabiki wa Simba kwa kumtungua Aishi Manula kwa bao la mpira wa adhabu uliozama wavuni baada ya kuchezewa rafu na Jonas Mkude nje kidogo ya 18.

Morrison amesema:-“Nafurahi kufanya kile ambacho ninakipenda kwani tulijiandaa vizuri na kila mchezaji alikuwa tayari kuona tunashinda na hicho ndicho kimetokea, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti,” .

Yanga imeifunga Simba mabao 3-2 msimu huu wa 2019/20 baada ya ule wa kwanza timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: MSIMU HUU USHINDANI NI MKUBWA