Home Uncategorized MTIBWA SUGAR: MSIMU HUU USHINDANI NI MKUBWA

MTIBWA SUGAR: MSIMU HUU USHINDANI NI MKUBWA


 THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ni mkubwa jambo ambalo linalowapa matokeo ya tofauti ndani ya uwanja.

Kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Novemba Mosi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba Mtibwa Sugar iliyeyusha pointi tatu mazima kwa kufungwa mabao 2-1 .


Licha ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuitungua Azam FC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 25 ilikwama kushinds mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Meck Maxme ambaye msimu huu mambo kwake ni magumu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kifaru amesema kuwa:”Ni ngumu kusema kwamba tumepoteana kwa sasa kwa kuwa ligi bado inaendelea na mechi ambazo tunazo ni nyingi.


“Bado kazi ipo hasa ukizingatia kwamba kila mchezaji ana morali kubwa ya kusaka ushindi ndani ya uwanja licha ya kwamba tunashindwa kupata matokeo.


“Ushindani kwa msimu huu ndani ya ligi ni mkubwa na huu ni mzuri kwa kuwa unafanya kila timu isijipe matumaini ya kupata matokeo kwenye mechi zake ikiwa haitafanya juhudi kusaka ushindi,” amesema.


Jana pia Novemba 5, Mtibwa Sugar iliangusha pointi tatu nyingine mbele ya Coastal Union kwa kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Moro.


Bao pekee la ushindi kwa Coastal Union lilipachikwa kimiani na Hamad Majimengi dakika ya 55 na kuwafanya wapoteze mchezo wa pili mfululizo ndani ya ligi.

SOMA NA HII  BREAKING: ZAHERA AFUNGIWA MECHI TATU KUITUMIKIA YANGA