Home Yanga SC NYOTA HAWA WANNE YANGA KUTOKUWEPO MSIMU UJAO

NYOTA HAWA WANNE YANGA KUTOKUWEPO MSIMU UJAO


 NYOTA wanne ndani ya Yanga wanahesabu siku tu kabla ya kufungashiwa virago ili kuweza kusepa kikosini hapo baada ya kushindwa kuonyesha kile ambacho kilitarajiwa.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ambaye alirithi mikoba ya Cedric Kaze kwa sasa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, kesho majira ya saa 2:15.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ndani ya kikosi hicho ni kufanya maboresho mapya kwa kuwaondoa wachezaji ambao hawana mchango mkubwa.

“Kweli kwa sasa Yanga ipo kwenye hesabu za kufanya maboresho ya kikosi hicho ambapo tayari wapo wachezaji ambao wameambiwa kwamba hawataongezewa mikataba hivyo wanasubiri siku za kuondoka.

“Fiston Abdulazack huyu mkataba wake unaisha kuongezewa mkataba wake ni ngumu, Michael Sarpong asibopadilika kwenye mzunguko huu wa pili basi safari inamuhusu.

“Farid Mussa amekuwa kwenye kiwango cha kawaida tofauti na ilivyotarajiwa, Wazir Junior naye hana maisha marefu na anaweza kutolewa kwa mkopo, hivyo msimu ujao hawa jamaa wanaweza kuwa na maisha sehemu nyingine” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  WINGA TELEZA WA TP MAZEMBE AKUBALI KUTUA YANGA...NI YULE ALIYEMTESHA ULIMI DJUMA