Home Uncategorized MKWASA ATOA ONYO YANGA JUU YA USAJILI WA WACHEZAJI KUPITIA YOUTUBE

MKWASA ATOA ONYO YANGA JUU YA USAJILI WA WACHEZAJI KUPITIA YOUTUBE


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kutoa rai kwa viongozi wa klabu hiyo juu ya usajili wanaoufanya hivi sasa.

Mkwasa ambaye hivi sasa bado anaugulia kutokana na tatizo la moyo lililomfanya aachie ngazi Yanga, ameamua kuweka wazi suala la usajili unaondelea klabuni hapo ambao unaenda kwa kasi.

Mkwasa amesema ni vizuri zaidi Yanga wakaangalia wachezaji ambao watakuwa na msaada ndani ya timu.

Amesema si vema kusajili wachezaji kupitia ‘KLIPU’ za YouTube maana haziamini na wengi kuwa wanazitengeneza.

“Ni vizuri Yanga wakasajili kwa kuangalizia vipaji na si YouTube.

“Klipu nyingi za YouTube zinakuwa ni za kutengenezwa hivyo ni vema wakawa makini zaidi.”

SOMA NA HII  NAIBU WAZIRI WA HABARI, SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI AKABIDHI KOMBE KWA MABINGWA WA NDONDO CUP UV TEMEKE