Home Uncategorized NAIBU WAZIRI WA HABARI, SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI AKABIDHI KOMBE KWA MABINGWA...

NAIBU WAZIRI WA HABARI, SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI AKABIDHI KOMBE KWA MABINGWA WA NDONDO CUP UV TEMEKE


NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Juliana Shonza amewakabidhi kombe la Ndondo Cup timu ya UV Temeke, yenye maskani yake Temeke jana baada ya kuwanyoosha wapinzani wao Uruguay.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Bandari ulikuwa ni wa kukata na shoka kwa timu zote kuhaha kutafuta matokeo.

Licha ya Uruguay kupachika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Chinu Mbaya halikudumu kwani UV Temeke waliweka mzani sawa kupitia kwa Hamis Ngoengo.

 
UV Temeke imetwaa ubingwa huo kwa ushindi wa penalti 5-3.

SOMA NA HII  NDAYIRAGIJE ATAKA MASHINE KALI NNE, ASHIKILIA JINA LA MZAWA MMOJA