Home Uncategorized NDAYIRAGIJE ATAKA MASHINE KALI NNE, ASHIKILIA JINA LA MZAWA MMOJA

NDAYIRAGIJE ATAKA MASHINE KALI NNE, ASHIKILIA JINA LA MZAWA MMOJA

SELEMAN Ndikumana raia wa Burundi anaungana na nyota wengine wapya ndani ya Azam FC ambao ni pamoja na Idd Seleman ‘Nado’ Emmanuel Mvuyekure ambaye naye ni raia wa Burundi kujiaanda kutetea kombe la Kagae litakalofanyika nchini Rwanda mwezi Julai.
Kwa sasa Azam FC wameanza kujiwinda kutetea kombe la Kagame ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Julai.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije hesabu zake ni kusajili nyota wakali wanne ndani ya kikosi hicho cha matajiri Bongo.
Wachezaji hao wawili ni wa nje na wawili wanapaswa wawe wa ndani ambapo tayari kwa wa nje ameshakamilisha mpango wake wa kwanza.
Mvuyekule na Ndikumana wanafunga usajili wa Ndayiragije kwa wachezaji wa nje na kubaki mchezaji mmoja wa ndani.
Nado ambaye ametoka Mbeya City ni mzawa ambaye amekuwa wa kwanza kusajiliwa msimu huu kwa maelekezo ya Ndayiragije.
Uongozi wa Azam FC, kupitia kwa Ofisa Habari, Jaffary Maganga umesema kuwa mchezaji huyo mmoja bado hajapendekezwa na kocha.
SOMA NA HII  MASHINE MPYA YA YANGA YAWAPOTEZA NYOTA WOTE SIMBA