Home Uncategorized MWINYI ZAHERA WA YANGA AGOMA KUREJEA BONGO

MWINYI ZAHERA WA YANGA AGOMA KUREJEA BONGO

LICHA ya timu yake kushindwa kufurukuta kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma kurudi mapema Bongo endapo atapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Zimbabwe.

Zahera kwa sasa yupo na kwenye benchi la ufundi la timu ya Congo akiwa ni kocha msaidizi na timu yake ipo mkiani kwenye kundi A baada ya kupoteza michezo yote miwili kwa kufungwa na Uganda pamoja na Misri.

Zahera amesema kuwa kwa sasa hafikirii kurejea Tanzania kuanza kukikonoa kikosi chake cha Yanga badala yake atakwenda Ufarasa kula bata na familia.

“Nimkekaa muda mrefu Tanzania nikiwa na timu yangu ya Yanga, kwa sasa sifikirii kurejea mapema kuanza maandalizi kwani ni muda wangu wa kupumzika na mke wangu.

“Mchezo wangu wa mwisho utakuwa tarehe 30 nina imani ya kufanya vizuri kwani tayari kwa sasa wachezaji wamepata uzoefu na nina imani ya kushinda kama tukipoteza basi nitakwenda zangu Ufarasa kupumzika na familia,” amesema Zahera.SOMA NA HII  YANGA :HAKUKUWA NA NAMNA GWAMBINA ILIKUWA LAZIMA ICHAPWE TU