Home Uncategorized EMMANUEL OKWI AIVURUGA SIMBA

EMMANUEL OKWI AIVURUGA SIMBA

NYOTA wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anazidi kuwa mtamu kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri amewavuruga mabosi wa Simba baada ya kutoweka wazi hatma yake ya kurejea Simba.

Okwi mpaka sasa kwenye michezo miwili ya Afcon ambayo Uganda wamecheza dhidi ya Congo pamoja na Zimbabwe amefunga mabao mawili na kuibuka mchezaji bora kwenye mchezo mmoja dhidi ya Congo hali inayomuongezea thamani.

Okwi amesema kuwa anajivunia kuwa na mashabiki wa Tanzania hali inayompa furaha hivyo wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa kwake kutaja hatma yake na Simba.

“Nafurahi kuwa na mashabiki wengi kutoka Tanzania nawapenda, kuhusu kurejea Simba kwa sasa ni ngumu kulizungumzia ila wakati ukifika itafahamika tu,” amesema Okwi.

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescetius Magori amesema kuwa kwa sasa wanafanya mazungumzo na wachezaji waliomaliza mkataba endapo watafikia makubaliano watawasainisha ili kuendelea kupata huduma zao.

SOMA NA HII  ISHU YA MRITHI WA MIKOBA YA SVEN NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI