Home Uncategorized AZAM FC KUKIWASHA LEO KOMBE LA MAPINDUZI

AZAM FC KUKIWASHA LEO KOMBE LA MAPINDUZI


 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina akiwa na msaidizi wake Vivier Bahati kitafungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kukipiga dhidi ya Mlandege, leo Alhamisi, Januari 7 kwenye Uwanja wa Amaan saa 2.15 usiku.


Mabingwa hao wa Kombe hilo la Mapinduzi waliwasili jana, Januari 6 wakiwa na kikosi kamili ambapo wameweka wazi kwamba malengo yao ni kutwaa ubingwa msimu huu ambao waliupoteza msimu wa 2020.

Rekodi zinaonyesha kuwa Azam FC imetwaa taji la Mapinduzi mara tano na mara ya mwisho ilikuwa msimu wa 2019 ambapo iliibamiza Simba mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

Msimu wa 2020 ilivuliwa ubingwa na Simba ambayo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo imeanza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chipukizi Januari 5, Uwanja wa Amaan.

Kocha Msaidizi, Bahati amesema kuwa kila kitu kipo sawa wanahitaji ushindi ili kufikia malengo ya kutwaa taji hilo la heshima.

“Tuna kikosi kizuri, wachezaji wanajituma na kila mmoja anapenda kutimiza majukumu yake hivyo ni wakati wetu wa kufanya kazi kile ambacho mashabiki wanahitaji pamoja na kuwapa burudani.
“Kila timu ambayo inashiriki ipo vizuri na ni jambo ambalo linafanya mashindano haya yazidi kuwa na ushindani, mashabiki wazidi kutupa sapoti tunaamini tutafanya vizuri,” .
SOMA NA HII  ZANA BADO YUPO SIMBA, UWEZO WAKE WAMKOSHA MBELGIJI, ISHU YA MKATABA YATAJWA