Home Uncategorized BEKI ALIYEKATALIWA NDANI YA SIMBA AWAUMBUA MABOSI ZAKE AKIWA YANGA

BEKI ALIYEKATALIWA NDANI YA SIMBA AWAUMBUA MABOSI ZAKE AKIWA YANGA


 LAMINE Moro, beki wa kati wa Klabu ya Yanga ambaye alipigwa chini alipofanya majaribio ndani ya kikosi cha Simba zama za Patrick Aussems kwa anachokifanya kwa sasa ni kama anawaumbua mabosi wa timu hiyo ambao walimkataa.

 

Habari zinaeleza kuwa Aussems ambaye alipewa jukumu la kupitisha jina la beki huyo kitasa raia wa Ghana alilipiga chini jembe hilo kwa kile alichokieleza kuwa uwezo wake ni mdogo.


 

Rekodi za mchezaji mmoja zinaonyesha kuwa Moro ndani ya Ligi Kuu Bara ni kinara wa utupiaji wa mabao kwa mabeki akiwa nayo manne na ana pasi moja ya bao pia ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Cedric Kaze na amempoteza yule wa Simba, Joash Onyango mwenye bao moja.


Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 na kuruhusu mabao 7 ya kufungwa, Moro amecheza mechi 15 na kukosekana kwenye mechi tatu ambapo moja alikosa kwa sababu ya kadi tatu za njano ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania.

 

Mechi 14, ameyeyusha dakika 90 na kumfanya atumie jumla ya dakika 1,260 na moja alitumia dakika 45 nayo kwa sababu aliumia ilikuwa dhidi ya Simba. 


Jumla ametumia dakika 1,305 ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 na timu yake ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia pointi 44 kibindoni.

 

Onyango wa Simba, timu yake ikiwa imeruhusu mabao matano, amecheza jumla ya mechi 14 kati ya 15, ambazo zimechezwa na mabingwa hao watetezi chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.


 Mechi 13, aliyeyuyusha dakika 90 na kufanya atumie jumla ya dakika 1,170 na alitumia dakika 68 kwenye mechi moja hivyo jumla ndani ya Ligi Kuu Bara amecheza mechi 14 na kutumia dakika 1,238.


Timu yake ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza jumla ya mechi 15 ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  STRAIKA MAN UNITED ATUA INTER MILAN