Home Habari za michezo BAADA YA PABLO ‘KUTUMBULIWA SIMBA’…KADUGUDA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA KUHOJI KOSA LAKE NI...

BAADA YA PABLO ‘KUTUMBULIWA SIMBA’…KADUGUDA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA KUHOJI KOSA LAKE NI LIPI…?


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ amehoji maamuzi ya Uongozi wa klabu hiyo kumfuta kazi Kocha Franco Pablo Martin.

Simba SC leo Jumanne (Mei 31) imetangaza rasmi kuachana na Kocha Pablo, kwa makubaliano ya kuvunja mkataba yaliofanywa na pande zote mbili.

Kaduguda ambaye hakuwa sehemu ya viongozi waliokwenda Mwanza kushuhudia mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans, amesema haoni sababu ya kocha Pablo kuondolewa.

Amesema Kocha huyo aliikuta Simba SC imeshafanya usajili na baadhi ya mambo mengine ya kiufundi, hivyo hakupaswa kufukuzwa kwa kigezo cha kushindwa msimu huu.

“Makocha wamekuwa wakitimuliwa bila sababu, mfano Pablo kafika katikati ya msimu timu kasajiliwa, anatimuliwa kwa kosa lipi? Je, kwenye makubaliano yake alivyokuwa anavihitaji mmemtekelezea?” amehoji Kaduguda

SOMA NA HII  KUELEKEA 'KARIKAOO DERBY'...BENCHIKHA AWAPA KISOMO MASTAA WOTE SIMBA...