Home Habari za michezo ‘KUTUMBULIWA’ KWA PABLO….MANARA NAYE AONYESHA MSHANGAO WAKE…AMTUPIA KOMBORA BARBARA…ATAJA MIGOGORO..

‘KUTUMBULIWA’ KWA PABLO….MANARA NAYE AONYESHA MSHANGAO WAKE…AMTUPIA KOMBORA BARBARA…ATAJA MIGOGORO..


Masaa machache tangu kutimuliwa Kwa Kocha wa Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club Pablo Franco Martin.

Aliyekuwa Afisa Habari wa Klabu ya Simba ambaye kwa sasa amehamia Upande wa Pili akiisemea Klabu ya Yanga, Haji Manara amemsikitikia Kocha huyo na kuweka wazi kile ambacho kimechangia kumfelisha Kocha huyo klabuni hapo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amepost picha akiwa na Pablo na kuandika;

“Kocha Bora mwenye nidhamu kubwa na mapenzi mazito na Football pamoja na Wachezaji wake anaondoka nchini.

Pamoja na kufanya kazi katika Mazingiza magumu ya kukosa Proper Management iliyogubikwa na Migogoro isiyoisha, Jamaa aliiwezesha Club yake kufika Robo fainali ya Shirikisho.

Binafsi ntammiss kwa uungwana wake na ucheshi wake.

Kila la kheri Rafiki yangu Pablo, Kwa msimu huu tu wewe ni Kocha wa pili kufukuzwa na naamini hadi msimu uishe tutasikia mengi.’

Kwa alichoandika Manara hapo, utaona wazi kuwa ametupa lawama kwa ‘menejimenti’ ya Simba, ambayo kiutawala iko chini ya Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez.

Hivyo ni sawa na kusema kuwa Manara amemtuhumu waziwazi kwa mara nyingine Bi Barbara kwa kumfukuza kazi Pablo, huku yeye Manara akiamini kuwa haikuwa sahihi.

SOMA NA HII  KABLA HUYAWEKA MKEKA MWINGINE ...ZINGATIA HILI JIPYA KUTOKA MERIDIANBET...