Home Uncategorized SIBOMANA WA YANGA APANIA MAKUBWA

SIBOMANA WA YANGA APANIA MAKUBWA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, aliyetupia tatu dhidi ya Moro Academy , Patrick Sibomana, amewaambia mashabiki kwamba ndiyo zake wala hakubahatisha wazisubiri nyingi Uwanja wa Taifa.
Amesisitiza kwamba, hata Township Rollers lazima wawapige si chini mabao matatu na kuendelea pale Taifa ili kuthibitisha kwamba wamerudi vizuri kimataifa.
Yanga ambao imefanya usajili wa aina yake msimu huu, itacheza na timu hiyo kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Kocha Mwinyi Zahera akitarajiwa kutua Dar es salaam leo Alhamisi akitokea kwao Ufaransa na kupitiliza moja kwa moja Morogoro.

Township ipo kambini Afrika Kusini na Yanga imejikita Morogoro. Katika ratiba hiyo, Yanga itaanzia nyumbani kucheza na Township Rollers ya Botswana kati ya Agosti 9 hadi 11, mwaka huu na kurudiana ugenini Agosti 23 hadi 25, mwaka huu.
Sibomana aliyejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Mukura Victory ya kwao Rwanda, amesema lazima washinde mchezo huo wa nyumbani kwa ushindi mnono ili wakienda ugenini kazi iwe rahisi.
“Tunaanzia nyumbani, ni kitu kizuri kwani mechi za nyumbani ni nzuri kuanza na ushindi, mkienda ugenini na ushindi, basi mnawapa shida wapinzani wenu.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO